KUKAMILIKA KWA MATENGENEZO KATIKA KITUO CHA KUSUKUMA MAJI WAZO NA KUREJEA KWA HUDUMA

Kazi ya matengenezo ya umeme katika kituo cha kusukuma maji Wazo yaliyodumu kwa muda wa Saa 48 yamekamilika.
Matengenezo yalihusisha mfumo wa kupokea umeme (33kV), kuondoa vipuli viilivyopata hitilafu na ufungaji wa vipuli vipya.
Kukamilika kwa matengenezo haya kumerejesha huduma ya Maji katika maeneo mbalimbali ambayo ni
Njia panda ya Kinzudi, Oysterbay, Mkomeni, Moga, Japhet, Matairi matatu, Frame nne Kibululu, Nassar, TripleB, Kisanga A, Kisanga B, Mafuriko, Bwawani, Bankimoon, Ipinda, Kontena, Umoja road, Zanzibar, Mashamba ya jeshi, Machimbo, Nakalekwa, Msigani, Uwata, Madale, Mivumoni center, Atlas, Valley view, Kisiwani, Kanjibah, Kulangwa, Mivumoni Kusini, Future, Vangameli na Dangote
Maeneo mengine ambayo huduma inaendelea kuimarika ni Tegeta A, Goba Mpakani, Uwanja wa Nike, Goba center, Modamba, Ulungwini, Lastanza, Kwa awadhi, Msikiti wa Pazi, Adora, na Serikali za mtaa Goba, Savana, Kwa bwege, Mji Mpya, Kwashufa, Hekima, Tanzania, Paris Bar, Matosa halisi, Shimbikati Matosa uzaramoni, Goba njia nne, Cha urembo, Uhuru road, Kwa Mathias Kilimanjaro, Ukawa, Mlimani city, Goba Mpakani, Upendo, Smart way, Jangwani, Posoa, Makarani, Wall paving Madawa, Madina na Msiri.