Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
MAANDALIZI KUZIMA MTAMBO WA MAJI RUVU CHINI SAA 14 YAMEKAMILIKA
08 Jun, 2025
MAANDALIZI KUZIMA MTAMBO WA MAJI RUVU CHINI SAA 14 YAMEKAMILIKA

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa  Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imesema maandalizi muhimu kwa ajili kufanya matengenezo ya miundombinu ya bomba kuu la inchi 30 katika Mtambo wa uzalishaji maji Ruvu chini ulioyopo wilayani Bagamoyo, mkoani Pwani yamekamilika.

Meneja Mtambo wa uzalishaji Maji Ruvu Chini, Mhandisi Tyson Mkindi ameeleza kuwa ni matengenezo ya dharura kwenye bomba kuu la kupokea Maji. 

"Timu ya ufundi imekamilisha maandalizi muhimu ya kuwezesha kazi ya matengenezo ambapo itakayopelekea kuzima mtambo wa Maji Ruvu Chini kwa wastani wa saa 14 i ili kufanikisha kazi hiyo" amebainisha Mhandisi Mkindi

Mhandisi Mkindi amesena kutokana na kuzimwa kwa kazi hiyo kutapelekea maeneo mbalimbali kukosa huduma ya maji ambayo ni: Bagamoyo, Mapinga, Mabwepande, Bunju, Tegeta, Mbweni, Boko, Kunduchi, Salasala, Goba, Mivumoni, Kawe,  Lugalo, Makongo,  Chuo - Kikuu Dar, Mwenge, Kijitonyama, Mikocheni, Msasani, Oysterbay,  Masaaki,  Upanga, Kariakok, Mwananyamala, Kinondoni, Magomeni, Kigogo, Chang'ombe,  Keko, Kurasini, Kigamboni, Airport, Kiwalani, Buguruni, Vingunguti,  Ilala na Katikati ya mji.