MAANDALIZI YA MWENGE WA UHURU 2025 WILAYA YA KINONDONI
31 May, 2025

Kamati ya siasa ya Manispaa ya kinondoni ikiongozwa na Mstahiki Meya Mheshimiwa Songoro Mnyonge imetembelea na kuridhishwa na maandalizi ya Mradi wa maji Mbopo-chekanao ambao ni mmojawapo ya miradi ya maendeleo itakayopitiwa na Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2025.
Mradi huo unategemea kunufaisha zaidi ya wakazi 2,000 wa mtaa wa Mbopo katika kata ya Mabwepande, Wilaya ya Kinondoni.
Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2025 unategemea kufika Mkoa wa Dar es Salaam na kukimbizwa katika Wilaya tano za Temeke, Ilala, Kinondoni, Ubungo na Kigamboni kuanzia tarehe 1.6.2025 hadi 6.6.2025.
Kukamilika kwa mradi huu kitanufaisha zaidi ya wakazi 2000 wa mtaa wa Mbopo, kata ya Mabwepande kayika Wilaya ya Kinondoni.