MABORESHO HUDUMA YA MAJISAFI KATA YA MLANDIZI-PWANI
20 Feb, 2025

Kazi ya matengenezo ya bomba la inchi 6 yakiendelea kutekelezwa na mafundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) katika eneo la Hai Village kwa lengo la kuongeza msukumo wa maji kwa wakazi wa mitaa ya Mlandizi Kati na Mlandizi Mjini katika Kata ya Mlandizi, Mkoani Pwani.
Wateja zaidi ya 900 katika maeneo ya Hai, Janga, Uwanja wa star, Kona pub, Msongola, Miti mirefu na Disunyara wanatarajiwa kupata huduma kwa msukumo mzuri baada ya kukamilika kwa kazi hii.
DAWASA inaendelea na kazi ya kuboresha usambazaji wa huduma ya majisafi kwa wananchi kwa lengo la kuimarisha upatikanaji wa huduma kikamilifu.