Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
MAJARIBIO UFUNGAJI MITA ZA MALIPO YA KABLA YASHIKA KASI
15 Jun, 2024
MAJARIBIO UFUNGAJI MITA ZA MALIPO YA KABLA YASHIKA KASI

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) inaendelea kwa kasi  na zoezi la ufungaji wa dira za majaribio za malipo ya kabla (pre-paid meters) ambapo hadi sasa dira zaidi ya 160 zimefungwa kwa wateja wakubwa na wadogo waliopo kwenye eneo la huduma.

Zoezi hili ni endelevu hadi sasa
Mamlaka imefunga dira hizo  katika hoteli kubwa, Taasisi za Serikali, Mabalozi na nyumba za viongozi wa Serikali katika Wilaya ya Kinondoni na Ilala.

Lengo kuu la kufunga dira hizo za majaribio ni kupima ufanisi wake kuelekea mabadiliko ya kuanza kutumia rasmi dira za huduma ya malipo ya kabla unaotazamiwa kuanza hivi karibuni.