MANZESE, SINZA HADI TANDALE WAENDELEA KUUNGANISHIWA HUDUMA ZA MAJISAFI

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kupitia mkoa wa kihuduma Magomeni imeendelea na zoezi la utoaji wa vifaa vya maunganisho mapya ya huduma ya majisafi kwa wananchi wa maeneo ya Manzese, Tandale hadi Sinza ili waweze kunufaika na jitihada za Serikali za kuhakikisha wamepata huduma ya majisafi.
Sambamba na zoezi la utoaji wa vifaa hivyo, DAWASA Magomeni imetoa elimu kwa wateja hao wapya kuhusu utunzaji wa miundombinu ya maji, matumizi sahihi ya maji, njia rasmi ya kimawasiliano, malipo ya ankara na huduma nyingine zitolewazo na Mamlaka.
Zaidi ya wateja wapya 25 wa maeneo ya Manzese, Tandale, Sinza, Magomeni na Kigogo wataanza kunufaika na huduma ya majisafi baada ya kukamilika kwa zoezi la maunganisho.
Mamlaka inawasisitiza wananchi wanaohitaji kuunganishiwa huduma ya ya majisafi kuwasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 0800110064 (Bila malipo) au 0735 451 862 DAWASA Magomeni.