Wizara ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)

TIRA Logo
MATENGENEZO HITILAFU YA BOMBA AFRIKANA KAZI INAENDELEA.
02 Nov, 2026
MATENGENEZO HITILAFU YA BOMBA AFRIKANA KAZI INAENDELEA.

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar Es Salaam (DAWASA) inaendelea na kazi ya matengenezo ya bomba lenye ukubwa wa inchi 8 eneo la Afrikana lililopata hitilafu na kupelekea kukosekana kwa huduma ya maji kwa wakazi wa kata ya Kawe.

Kukamilika kwa kazi hii kutaimarisha huduma ya maji katika maeneo ya Mbezi Beach A na Mbezi Beach B yaliyoathiriwa na matengenezo haya ya dharura.

Matengenezo haya yaliyoanza mapema Oktoba 31,2026 yanatarajia kukamilika ifikapo saa 10 Jioni Leo Nov 1, 2026.