Wizara ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)

TIRA Logo
MATENGENEZO HITILAFU YA BOMBA JANGWANI KAZI INAENDELEA.
29 Oct, 2026
MATENGENEZO HITILAFU YA BOMBA JANGWANI KAZI INAENDELEA.

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar Es Salaam (DAWASA) inaendelea na kazi ya matengenezo ya bomba lenye ukubwa wa inchi 16 eneo la Jangwani lililopata hitilafu na kupelekea kukosekana kwa huduma ya maji kwa wakazi wa Muhimbili hadi Magomeni.

Kukamilika kwa kazi hii kutaimarisha huduma ya maji katika maeneo ya Hospitali ya Taifa Muhimbili, Taasisi ya mifupa MOI,  Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS), Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Upanga, Kariakoo, Magomeni Dosa, Magomeni eneo la Ubungo, Jangwani na kiwanda Cha TBL.

Matengenezo haya yamefanyika kwa muda wa Saa 10 yaliyoanza mapema Oktoba 28,2026 yanatarajia kukamilika ifikapo saa 2 usiku.