Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
MAUNGANISHO YA MAJI DAWASA YASHIKA KASI
16 Jun, 2025
MAUNGANISHO YA MAJI DAWASA YASHIKA KASI

Zaidi ya Kaya 47 zaunganishiwa huduma kwa wakati Tegeta 

Kaya 47 kutoka maneno mbalimbali katika kata nne za Kunduchi, Wazo, Bunju na Mbweni wamenufaika na zoezi la maunganisho mapya ya huduma ya Majisafi yanayoendelea katika mkoa wa kihuduma DAWASA - Tegeta.

Akizungumza wakati wa utoaji wa vifaa vya maunganisho mapya, Mhandisi wa Miradi DAWASA-Tegeta James Sinare ameeleza kuwa zoezi hili ni endelevu na wananchi waendele kujitokeza kupatiwa huduma ya maji.

"Wale wote waliotuma maombi wa huduma na kulipia gharama za maunganisho tunaendelea kuwapatia vifaa na kuwaungia huduma ya maji, niwasihi wananchi zaidi kutuma maombi na kufanya malipo ili tuweze kuwafikishia huduma ya majisafi" ameeleza Mhandisi Sinare

Sinare ameongeza kuwa zoezi hili ni endelevu na kila mwananchi alieomba huduma ya majisafi atapatiwa huduma hiyo Kwa haraka na wakati.

Ndugu, Easther Tarimo mkazi wa Basihaya ameonyesha kuridhishwa na kasi ya DAWASA kuwakishia huduma ya majisafi na kuwasihi wananchi ambao bado hawajapata huduma kujitokeza kupatiwa huduma hiyo.

"DAWASA wanafanya kazi kubwa sana, wakazi wengi tuliopo leo hapa tumefanya malipo ya maunganisho ya majisafi siku zisisozidi 3 na Leo tumepata vifaa na kuunganishwa na huduma ya maji, naomba kasi hii isipungue ili wananchi wengi tuondokane na adha ya kutokua na huduma ya majisafi" ameeleza ndugu Easther.

Sambamba na ugawaji wa vifaa vya maunganisho mapya, DAWASA imetoa elimu juu ya huduma mbalimbali zinazotolewa na Mamlaka ikiwemo, ulipaji wa ankara za maji kwa wakati, njia za malipo pamoja na utunzanji wa miundombinu ya majisafi.