Wizara ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)

TIRA Logo
MHANDISI MKAMA BWIRE AONGOZA WATUMISHI WA DAWASA KUMUAGA MAREHEMU GIDEON MINJA
11 Nov, 2026
MHANDISI MKAMA BWIRE AONGOZA WATUMISHI WA DAWASA KUMUAGA MAREHEMU GIDEON MINJA

Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) Mhandisi Mkama Bwire ameongoza watumishi wa DAWASA katika kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Gideon Minja, aliyekuwa Afisa Tehama DAWASA Mwananyamala,Marehemu Gideon Minja alifariki dunia tarehe 6 Novemba 2026 katika Hospitali ya Bochi Kimara Dar es salaam.

Watumishi wa Mamlaka wameungana na familia, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu kutoa heshima za mwisho katika kanisa la Parokia ya Mtakatifu Ritha Goba, Mwili wa marehemu utasafirishwa kuelekea Moshi kwa ajii ya kupumzishwa katika makaburi ya KCMC tarehe 11 Novemba 2026.
 
Katika kipindi chote cha utumishi wake,Marehemu Gideon Minja alitambulika kama mtumishi mwenye bidii,weledi,nidhamu na uwajibikaji katika kutekeleza majukumu yake, Alikuwa mtu wa kujituma, mwenye ushirikiano mzuri na wenzake pamoja na kujitoa katika kuhakikisha malengo ya Mamlaka yanafikiwa.Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.