Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
MRADI WA MAJI BANGULO WAIKUZA PUGU STESHENI KIUCHUMI
30 Jul, 2025
MRADI WA MAJI BANGULO WAIKUZA PUGU STESHENI KIUCHUMI

Wakazi mbalimbali kutoka mtaa wa Pugu station, Kata ya Pugu station Wilaya ya Ilala wameishukuru Serikali ya Awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutenga fedha za utekelezaji wa mradi wa maji Bangulo ambao kukamilika kwakwe kumekwamua shughuli mbalimbali za kimaendeleo.

Mradi huu unaogharimu kiasi cha shilingi bilioni 36.9 unahudumia majimbo matano ya uchaguzi ya Ukonga, Segerea, Ubungo, Temeke na Kisarawe ambapo hadi sasa umeanza kuleta matokeo chanya katika maeneo hayo

Ndugu Said Gobere mkazi wa mtaa wa Pugu station ameeleza kuwa hapo awali walilazimika kufuata huduma ya maji zaidi ya Kilomita 5, jambo ambalo lilikwamisha kazi nyingi za kimaendeleo katika mtaa wao na kuwarudisha nyuma kiuchumi.

"Mradi huu ni neema kwetu, sasa maji tunayaona kila siku, shughuli zetu mbalimbali za kimaendeleo kama vile ujenzi na kilimo cha mbogamboga tulizozisimamisha sasa zinaendelea na tunajipatia kipato na kuinua uchumi wetu Tena" ameeleza Gobere.

Nae Aisha Ally mkazi wa mtaa wa Pugu station ameeleza kuwa adha waliyoipata kina mama majumbani siku za nyuma kutokana na ukosefu wa huduma ya majisafi, sasa imekwisha na shughuli zote za majumbani zinafanyika kwa wepesi.

"Tulikua tunalazimika kuweka ratiba ya kufua na hata kuosha vyombo kutokana na ukosefu wa maji majumbani, lakini sasa maji ni mengi, shughuli zote kama kufua, kuosha vyombo, kupika, kunyeshea mimea sasa zinafanyika kwa wakati na tunapata muda mzuri wa kukaa na familia zetu badala ya kutumia muda mwingi kutafuta huduma ya maji" ameeleza Aisha.

Kwa upande wake kaimu mwenyekiti wa mtaa wa Pugu station Bi. Tunza Mkandama ameeleza kuwa adha waliyoipata wananchi wa mtaa wake kwa kutumia maji chumvi waliyoyanunua kwa gharama kubwa kutoka visima vya watu binafsi imekwisha kabisa, huku tatizo la kupata maji mara moja kwa wiki likiwa limetatuliwa na sasa wanashirikiana na DAWASA kumaliza tatizo la mivujo ambayo inaashiria uwepo wa maji yenye msukumo mkubwa.