Wizara ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)

TIRA Logo
NAIBU WAZIRI KUNDO AANZA ZIARA YA SIKU 3 DAWASA
27 Nov, 2026
NAIBU WAZIRI KUNDO AANZA ZIARA YA SIKU 3 DAWASA

Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Andrew Mathew Kundo (Mb) ameanza ziara ya Siku tatu Mkoani Dar es salaam kukagua hali ya upatikanaji huduma ya Maji na utekelezaji wa miradi ya Maji inayosimamiwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA).

Mhe Kundo amepokelewa na Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Mkama Bwire pamoja na viongozi mbalimbali wa Wizara ya Maji na  ofisi za Mamlaka eneo la Mwananyamala.

Katika siku ya kwanza ya ziara yake Mheshimiwa Kundo atapokea taarifa ya uzalishaji na usambazaji Maji pamoja na kutembelea vyanzo vya Maji katika Mitambo ya Ruvu Juu na Ruvu Chini.