Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
"ONGEZENI KASI UTEKELEZAJI WA BWAWA LA MAJI KIDUNDA" - Mhandisi Mwajuma Waziri
09 Dec, 2024
"ONGEZENI KASI UTEKELEZAJI WA BWAWA LA MAJI KIDUNDA" - Mhandisi Mwajuma Waziri

Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Mwajuma Waziri amekagua utekelezaji wa Mradi wa Bwawa la Maji Kidunda na kumtaka Mkandarasi anayetekeleza mradi wa huo Kampuni ya Sinohydro Ltd kuongeza kasi ya ujenzi wa mradi huo na kuukamilisha kwa wakati ili kufikia malengo ya Serikali ya Awamu ya Sita kuhakikisha inakamilisha mradi ili kupunguza changamoto ya maji katika mikoa ya Morogoro, Pwani na Dar es salaam.

Mhandisi Mwajuma ameyasema hayo katika ziara yake ya kutembelea na kukagua ujenzi wa Bwawa hilo linalotarajia kuhifadhi maji kiasi cha mita za ujazo Milioni 190 pindi litakapo kamilika.

"Tunashukuru utekelezaji unaenda vizuri na juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan zinaonekana, fedha tayari zipo ni muda sasa wa mkandarasi kufanya kazi ili wananchi wanufaike na hili Bwawa la Kidunda" amesema