Wizara ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)

TIRA Logo
RUVU JUU KUFANYIWA MATENGENEZO YA KINGA KWA SAA 12, KIBAHA HADI KISARAWE KUKOSA HUDUMA
10 Sep, 2026
RUVU JUU KUFANYIWA MATENGENEZO YA KINGA KWA SAA 12, KIBAHA HADI KISARAWE KUKOSA HUDUMA

‎Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imezima Mtambo wa Ruvu Juu ulioko Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani na kupelekea kukosa huduma ya maji kwa takribani saa 12 katika maeneo ya Dar es Salaam na Pwani, leo Alhamisi, Septemba 10, 2026.
‎
‎Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano DAWASA, Bi Everlasting Lyaro amesema matengenezo yameanza kuanzia saa 12:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni, na sababu ni matengenezo kinga ya miundombinu ya maji katika Mtambo wa Ruvu Juu uliopo Kibaha, yanayolenga kujiandaa kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mvua kubwa zinazotarajiwa.
‎
‎Amesema maeneo yanayoathirika kutokana na matengenezo haya ni pamoja na Ruvu Darajani, Ruvu JKT, Vigwaza, Mlandizi, Mbwawa, Soga, Mwendapole, Tanita, Kwa Mathias, Picha ya Ndege, Kibaha, Kiluvya, Kibamba, Malamba Mawili, Saranga, Mbezi, Ubungo, Kimara, Tabata, Segerea, Kinyerezi, Kisukuru, Bonyokwa, Ukonga, Uwanja wa Ndege, Kiwalani, Vingunguti, Gongo la Mboto, Pugu na Kisarawe.
‎
‎Mamlaka imewataka Wananchi wa maeneo hayo kuhifadhi maji ya kutosha kwa matumizi muhimu wakati wa matengenezo, huku ikiomba ushirikiano wao ili kazi hiyo ikamilike kwa ufanisi.

‎