TUNASAFISHA MIFUMO YA MTANDAO WA MAJITAKA
Mafundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar Es Salaam (DAWASA)wakiendelea na kazi ya kuboresha Usafi wa Mazingira kwa kusafisha miundombinu ya majitaka na kuboresha chemba za ukusanyaji majitaka sehemu mbalimbali za Jiji, ikiwa ni jitihada za kukabiliana na uchafuzi wa Mazingira unaosababishwa na utiririkaji holela wa majitaka mitaani.
Mamlaka inaendelea kusisitiza matumizi sahihi ya miundombinu ya majitaka, kwa kuepuka kutupa taka ngumu kama vile nguo, mifuko ya plastiki, mawe na matairi, vile vile kuepuka kujiunganisha kiholela katika mifumo ya majitaka kwani kufanya hivyo ni makosa.
Uboreshaji wa miundombinu ya majitaka unaiepusha Jamii na hatari ya milipuko ya magonjwa kama vile kipindupindu. Wananchi wanasisitizwa kuwa walinzi wakwanza kwa kutoa taarifa wanapoona uhujumu wa miundombinu ya majitaka au utiririkaji wa maji hayo mitaani.
