UDHIBITI UPOTEVU WA MAJI MBEZI JUU
15 Jul, 2025

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kupitia Mkoa wa Kihuduma Kawe imetekeleza kazi ya udhibiti wa upotevu wa maji katika eneo la Baraza la Mitihani, Mbezi Juu.
Kazi hii imehusisha kubadilisha kipande cha bomba kilichoathirika katika bomba la usambazaji maji lenye ukubwa wa kipenyo cha inchi 6 katika eneo hilo.
Kukamilika kwa kazi hii kuataimarisha na kurejesha Huduma ya maji kwa wakazi wa Mtaa wa seni, Mtaa wa Msafiri, Ndumbwi, Baraza la mitihani, Mbezi juu Kati, Vose hotel, Mtaa wa mgogo, Kanisa la Sabato, Twiga street na Power nyati. Udhibiti wa Upotevu wa maji ni moja kati ya vipaumbele muhimu vya Mamlaka katika kuhakikisha inatoa huduma bora na endelevu kwa wananchi.