Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
UDHIBITI UPOTEVU WA MAJI MBEZI MAKABE, KAZI INAENDELEA
07 May, 2024
UDHIBITI UPOTEVU WA MAJI MBEZI MAKABE, KAZI INAENDELEA

Kazi ya kudhibiti  upotevu wa maji katika bomba la inchi 8 lililoathiriwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katik eneo la Mto Lubomwe imetekelezwa na mafundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA)

Kukamilika kwa kazi hii kumeimarisha upatikanaji wa maji kwa wakazi wa maeneo ya Makabe polisi, Makabe serikali ya Mtaa, Kwa Washa, Efatha, Msamaria, Kwa Mzungu, Kwa Biligenda, Dubai, Nyota njema na Kwa Fungo wilaya ya Ubungo.

DAWASA inaendelea kuwasihi wananchi kutoa taarifa endapo watabaina uvujaji katika maeneo yao mawasiliano rasmi ya Mamlaka kupitia Kituo cha huduma kwa wateja kwa 0800110064(bure)  na mitandao ya kijamii.