USOMAJI MITA SHIRIKISHI UNAENDELEA KIBAHA
11 Feb, 2025

Watumishi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mkoa wa kihuduma Kibaha wakiendelea na zoezi la usomaji mita kwa kushirikiana na wateja kwa lengo la kuboresha huduma katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Kihuduma.
Zoezi hili linaenda sambamba na utoaji elimu mbalimbali juu ya huduma zinazotolewa na DAWASA, ikiwemo uhakiki wa usomaji mita, njia za malipo na mawasiliano rasmi ya Mamlaka.
Mamlaka inaomba ushirikiano kwa Wananchi pindi Watumishi watakapopita katika makazi yao kwa kutekeleza zoezi hili.