Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
USOMAJI MITA SHIRIKISHI UNAENDELEA MKOA WA KIHUDUMA DAWASA KIBAMBA
12 Nov, 2024
USOMAJI MITA SHIRIKISHI UNAENDELEA MKOA WA KIHUDUMA DAWASA KIBAMBA

Watumishi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira (DAWASA) wa Mkoa wa Kihuduma DAWASA Kibamba wakiendelea na zoezi la usomaji mita shirikishi katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa kihuduma.

Zoezi la usomaji mita linaendelea kutekelezwa na DAWASA kwa kuwafikia wateja na kushirikiana katika usomaji wa mita za maji kwa lengo la kuboresha huduma. Aidha, zoezi hili huenda sambamba na utoaji wa elimu mbalimbali juu ya huduma zitolewazo na DAWASA ikiwemo uhakiki wa usomaji mita, njia za malipo na mawasiliano rasmi ya Mamlaka.

Mamlaka inaendelea kuomba ushirikiano pindi watumishi wa DAWASA watakapopita mtaani kwako kutekeleza zoezi hili.