WAKAZI MBAGALA KUU HADI KIBURUGWA KUANZA KUNUFAIKA NA HUDUMA YA MAJISAFI

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam kupitia mkoa kazi wa kihuduma DAWASA Mbagala imeendesha zoezi la ugawaji na utoaji wa vifaa vya maunganisho mapya ya huduma ya majisafi kwa wateja wa maeneo ya Mbagala Rangi Tatu, Mbagala Kuu, Kijichi, Kilungule, Mianzini, Kiburugwa, Chamazi, Kibondemaji, Charambe na Kiburugwa.
Mbali na zoezi la utoaji vifaa hivyo, DAWASA Mbagala imetoa elimu mbalimbali ikiwa ni pamoja na elimu ya utunzaji miundombinu ya maji, matumizi sahihi ya maji, njia rasmi za kimawasiliano, malipo ya ankara na huduma nyingine zitolewazo na DAWASA.
Jumla ya wateja wapya wapatao 50 wa maeneo hayo wanatarajia kuanza kunufaika na huduma ya majisafi baada ya kukamilika kwa zoezi la maunganisho.
Kwa msaada zaidi wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja namba 0800110064 (Bure) au 0734 302 352 DAWASA Mbagala.