Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
MSONGOLA JUU MAJI MWA MWA MWAA
29 Jul, 2025
MSONGOLA JUU MAJI MWA MWA MWAA

Zaidi ya wakazi 1,000 wa Kata ya Mlandizi katika kijiji cha Msongola Juu, Wilaya ya Kibaha Vijijini, Mkoa wa Pwani wameishukuru Serikali kwa uamuzi wa kupeleka mradi wa kusambaza maji kwenye maeneo yao kwa lengo la kuwaondolea changamoto ya upatikanaji wa huduma. 

Akizungumza mara baada ya kuanza kwa utekelezaji wa mradi huu, Mwenyekiti wa kijiji cha Msongola Juu, Ndugu Ayubu Lugongo amesema Serikali imefanya uamuzi mzuri kwa kuwaletea huduma ya maji wakazi hao ambao walikuwa kwenye dimbwi kubwa la upatikanaji wa maji.

Amesema mradi huu unaleta furaha kubwa kwa wananchi wote kwa kuwa walikuwa wanatumia maji ya kisima ili waweze kukidhi mahitaji yao. 

"Kwa jitihada hizi nipende kuishukuru na kuipongeza Serikali kwa kushirikiana na DAWASA na kuleta mradi huu unaotusaidia kupunguza malalamiko ya wananchi kuhusu hali ya maji," amesema Ndugu Lugongo akisisitiza, waliteseka lakini sasa wanafurahia. 

Kwa upande wake, Msimamizi wa mradi, Mhandisi Ally Migeyo amesema mradi umelenga kunufaisha wakazi wa Msongola na maeneo ya jirani walio kwenye uhaba wa maji. 

Amebainisha utekelezaji wa mradi umehusisha kazi ya ulazaji wa mabomba ya inchi 4 na 3 kwa umbali wa kilomita 7.2. 

Amesema kuwa mradi utanufaisha Kata hii pamoja na Kata ya Mlandizi kwenye vitongoji vya Sunguti, Kawawa, mji mwema, Upendo, Msufini na Msongola Juu. 

Mhandisi ameongeza awali eneo hili halikuwa na chanzo cha huduma ya maji, wananchi walikuwa wanapata huduma kutoka maeneo jirani, lakini kwa sasa wataenda kunufaika na huduma ya maji moja kwa moja majumbani mwao. 

Mhandisi Migeyo amewataka wananchi kulinda miundombinu ya maji ambayo Serikali imetumia gharama kubwa ya kuijenga kwa lengo la kufikisha huduma ya maji katika maeneo yao. 

Mkazi wa Kata ya Msongola Ndugu Oscar Balitazari ametoa shukrani za dhati kwa Mhe. Mama Samia kwa watu wa Msongola juu, tulikuwa tunapata maji kutoka Vijiji vya jirani na maji yenyewe ni ya visima, kwa mradi huu tunashukuru sana DAWASA na usimamizi wake.