Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
WAKAZI TANDALE - SINZA KUANZA KUFURAHIA MATUNDA YA SERIKALI KUWAFIKISHIA MAJISAFI
13 Nov, 2024
WAKAZI TANDALE - SINZA KUANZA KUFURAHIA MATUNDA YA SERIKALI KUWAFIKISHIA MAJISAFI

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kupitia Mkoa wa kihuduma Magomeni imeendesha zoezi la utoaji wa vifaa vya maunganisho mapya ya majisafi kwa wateja wa maeneo ya Tandale, Manzese, Makurumla, Kigogo, Tabata Dampo, Mabibo, Magomeni, Ndugumbi na Sinza, ili wanufaike na jitihada za Serikali za kuhakikisha wanapata maji.

Mbali na zoezi la utoaji wa vifaa hivyo, DAWASA Magomeni imetoa elimu mbalimbali ikiwa ni pamoja na elimu ya utunzaji miundombinu ya maji, matumizi sahihi ya maji, njia rasmi za kimawasiliano, malipo ya ankara na huduma nyingine zitolewazo na DAWASA.

Jumla ya wateja wapya 55 wa maeneo hayo wanaenda kunufaika na huduma ya majisafi baada ya kukamilika kwa zoezi la maunganisho.

Kwa msaada zaidi wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 0800110064 (Bure) au 0735 451 862 DAWASA Magomeni.