WANANCHI WASHUHUDIA UZINDUZI WA MRADI WA MAJI MBOPO CHEKANAO
04 Jun, 2025

Wananchi mbalimbali wamejitokeza kwa wingi katika shule ya Msingi Mbopo kushuhudia tukio la Mwenge wa Uhuru Kitaifa utakapotembelea na kuzindua Mradi wa maji Mbopochekanao uliotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA).
Mradi wa maji Mbopochekanao umegahrimu kiasi cha shilingi milioni 280 na utanufaisha wakazi zaidi ya 2000 pamoja na taasisi za Serikali kama vile shule zinazopatikana mtaani hapo.