WANANCHI ZAIDI YA 35 KISARAWE WAUNGANISHIWA HUDUMA YA MAJI SAFI

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kupitia Mkoa wa kihuduma DAWASA Kisarawe imeendelea na zoezi la utoaji wa vifaa vya maunganisho mapya ya majisafi kwa wananchi wa maeneo ya Sanze, Kimani, Umatumbini, Kinyamwezi na Kisopwa ili waweze kunufaika na jitihada za Serikali za kuhakikisha wanapata huduma ya maji safi.
Sambamba na zoezi la utoaji wa vifaa hivyo, DAWASA Kisarawe imetoa elimu kwa wateja hao wapya kuhusu utunzaji miundombinu ya maji, matumizi sahihi ya maji, njia rasmi za kimawasiliano, malipo ya ankara na huduma nyingine zitolewazo na Mamlaka.
Zaidi ya wateja wapya 35 wa maeneo hayo wataanza kunufaika na huduma ya majisafi baada ya kukamilika kwa zoezi la maunganisho.
Kwa msaada zaidi wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 0800110064 (Bure) au 0738 096 085 DAWASA Kisarawe.