WATEJA 275 WAFUNGIWA HUDUMA YA MAJISAFI CHALINZE
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mkoa wa Kihuduma Chalinze imeendesha zoezi la ugawaji wa vifaa vya maunganisho mapya kwa wateja wapya 275 wa Mji wa Chalinze.
Wananchi walioomba huduma ya maji kutoka katika maeneo ya Bwilingu, Pera, Chamakweza, Magindu,Tawalanda, Msolwa, Mdaula, Ubena, Msoga, Mboga, Lugoba, Msata, Kiwangwa, Fukayosi, Miono, Mandera,
Kimange na Mbwewe
wamepokea vifaa hivyo na zoezi la kuunganishia wateja hao linaendelea.
Mamlaka inaendelea na zoezi la ugawaji wa vifaa vya maunganisho mapya kwa wateja wote walioleta maombi ya kupatiwa huduma ya majisafi katika maeneo yote yanayohudumiwa na DAWASA Dar es Salaam na Pwani.
Kwa msaada na taarifa zaidi wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja namba 0800110064 (Bure) au 0752 801178 (DAWASA Chalinze).