WATEJA WATAKIWA KUZINGATIA ULIPAJI BILI KWA WAKATI
20 Feb, 2026
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inaendelea kwa zoezi la kuhamasisha ulipaji wa ankara za maji kwa wateja wake katika maeneo ya kihuduma, ikiwa ni sehemu ya juhudi zenye lengo la kukusanya mapato na kuimarisha upatikanaji wa huduma bora na endelevu za majisafi na usafi wa mazingira.
Zoezi hili linalenga kuongeza ufanisi katika makusanyo ya mapato ili kuwezesha matengenezo ya miundombinu, upanuzi wa huduma, na uhakika wa maji kwa wananchi wote.
DAWASA inasisitiza kuwa ulipaji wa bili kwa wakati ni wajibu wa kila mteja na ni mchango muhimu katika kuhakikisha huduma za maji zinaendelea kutolewa kwa ubora, uhakika na ufanisi kwa manufaa ya jamii nzima.
