WAZIRI AWESO AWASILI KIKAO KAZI CHA DAWASA KUIMARISHA HUDUMA ENDELEVU ZA MAJI DAR
23 Feb, 2026
Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amewasili katika Kikaokazi cha Viongozi Waandamizi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kinacholenga kuandaa mikakati imara ya usimamizi na utoaji huduma endelevu za maji kwa wananchi katika Mikoa ya Dar es Salaam na baadhi ya maeneo ya Pwani.
Waziri Aweso ameambatana na Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Mwajuma Waziri, Naibu Katibu Mkuu, Bi Rose Ambrose pamoja na Menejimenti ya Wizara ya Maji.
