Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
WAZIRI AWESO ZIARANI KOREA KUSINI UBORESHAJI USAFI WA MAZINGIRA
09 Dec, 2024
WAZIRI AWESO ZIARANI KOREA KUSINI UBORESHAJI USAFI WA MAZINGIRA

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amewasili nchini Korea Kusini kwa mualiko maalum wa Benki ya Exim ya Korea na Mfuko wa Mashirikiano ya Kiuchumi wa Korea (EDCF) ambapo anatarajia kukutana na Makamu wa Rais wa Benki hiyo tarehe 06 Desemba, 2024 kujenga mashirikiano zaidi baada ya uwekezaji wa serikali ya Korea Kusini katika miradi ya Majitaka kwa Majiji ya Dar es Salaam, Dodoma na Manispaa ya Iringa.

Mhe. Aweso amepokelewa na mwenyeji wake Mheshimiwa Togolani Edriss Mavura, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Korea Kusini.

Aidha, akiwa nchini Korea Kusini, Mhe. Aweso ametembelea moja ya makampuni makubwa ya Teknolojia katika Sekta ya Maji nchini Korea ya Green Tech Inc. ambayo imefunga mfumo wa mita janja (Smart Water Management System) katika Manispaa 43 nchini humo pamoja na nchi nyingine, ili kujionea Teknolojia hiyo pamoja na kuona Mfumo huo unavyofanya kazi. 

Mhe. Aweso amesema kuwa Mamlaka ya Maji Iringa (IRUWASA) imepanga kufunga "Mfumo janja wa kusimamia Menejimenti ya Usambazaji Maji" Mjini Iringa (Smart Water Management System). 

Mradi huu utawezesha kupunguza upotevu wa maji na kusimamia ubora na msukumo wa maji katika mfumo wote wa usambazaji kupitia mfumo maalum wa mawasiliano.