WIKI YA MAJI YAUNGANISHA WATEJA WAPYA 50 KINONDONI

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kupitia Mkoa wa kihuduma Kinondoni inaendelea na zoezi la utoaji wa vifaa vya maunganisho mapya ya majisafi kwa wateja wa maeneo ya Makumbusho, Mwananyamala, Kambangwa, Hananasifu, Mikocheni, Msasani na Kinondoni ili wanufaike na jitihada za Serikali za kuhakikisha wanapata huduma ya maji.
Sambamba na zoezi la utoaji wa vifaa hivyo, DAWASA Kinondoni imetoa elimu mbalimbali ikiwa ni pamoja na elimu ya utunzaji miundombinu ya maji, matumizi sahihi ya maji, njia rasmi za kimawasiliano, malipo ya ankara na huduma nyingine zitolewazo na Mamlaka.
Zaidi ya wateja wapya 50 wa maeneo hayo wataanza kunufaika na huduma ya majisafi baada ya kukamilika kwa zoezi la maunganisho.
Maadhimisho ya Wiki ya Maji yatafikia kilele tarehe 22 Machi, 2025 yakibeba kaulimbiu isemayo "Uhifadhi wa Uoto wa Asili kwa Uhakika wa Maji."
Kwa msaada zaidi wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 0800110064 (Bila Malipo) au 0735 451 863 (DAWASA Kinondoni)