TAARIFA KWA UMMA - KUENDELEA KWA MATENGENEZO YA DHARURA KATIKA KITUO CHA KUSUKUMA MAJI SALASALA
TAARIFA KWA UMMA
KUENDELEA KWA MATENGENEZO YA DHARURA KATIKA KITUO CHA KUSUKUMA MAJI SALASALA
26.2.2025
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inawataarifu Wateja na Wananchi wanaohudumiwa Tenki la Maji Salasala kuwa, maboresho ya Dharura yanaendelea na hivyo kupelekea kukosekana kwa huduma ya maji kwa wateja wa eneo la Kawe na Mivumoni.
Muda; Matengenezo yanatarajia kukamilika leo Februari 26, 2025.
Sababu: Kuruhusu Maboresho ya dharura ya Mashine za kusukuma maji katika kituo cha Salasala
Maeneo yatakayoathirika ni; Kilimahewa , Kilimahewa juu, Kinzudi ,Majengo, Muungano, Ng’ombe road, Kwa abarikiwe, Tatedo, Kaburi moja, Wakutiri na Salasala Magengeni, Umoja street Kinzudi, Shamba la mzungu, Abarikiwe street, Ndumbwi street, Power nyati street, Azimio street, Usukumani, Umanyema Street, Kessy Street,Oraa street, Tatedo, Saleko street, Tanzanite street, Kunguru street, Mwakapala street, Mwaikambo Road na Forest Road
Tunaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza.
Kwa mawasiliano zaidi tupigie:
Kituo cha huduma kwa wateja 0800110064 (bure) au 0735 202121 (WhatsApp Tu)
Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano