Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
TAARIFA KWA UMMA - KUFUNGULIWA KWA MABWAWA YA MAJITAKA AIRWING - UKONGA
01 Oct, 2024 Pakua

TAARIFA KWA UMMA

KUFUNGULIWA KWA MABWAWA YA MAJITAKA AIRWING - UKONGA

30/9/2024

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inawatangazia Wananchi na Watoa huduma ya Magari ya uondoshaji Majitaka kuwa, Mabwawa ya kuchakata Majitaka Airwing yaliyopo eneo la Banana katika Wilaya ya Ilala yatafunguliwa kutoa huduma rasmi Oktoba 1,2024.

Magari yatakayotoa huduma katika eneo hili ni yale tu yaliyosajiliwa na kuwa na stika Maalumu kutoka DAWASA.

Kwa taarifa zaidi wasiliana nasi kituo cha huduma kwa wateja 0800110064 (Bure) au 0735 202 121 (WhatsApp tu)

Imetolewa na 

Kitengo cha Mawasiliano