TAARIFA KWA UMMA - KUKAMILIKA KWA MATENGENEZO KINGA KATIKA MTAMBO WA RUVU CHINI
14 Mar, 2025
Pakua
TAARIFA KWA UMMA
KUKAMILIKA KWA MATENGENEZO KINGA KATIKA MTAMBO WA RUVU CHINI
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inawatangazia Wananchi na Wateja wote kuwa Matengenezo Kinga yaliyofanyika leo Alhamisi, Machi 13, 2025 kuanzia saa 12:00 asubuhi katika Mtambo wa Ruvu Chini yamekamilika.
Matengenezo yamekamilika na huduma inaendelea kuimarika katika maeneo mbalimbali ya kihuduma.
Maeneo yanayohudumiwa na Mtambo wa Ruvu Chini na huduma kuimarika ni Wananchi kuanzia eneo la Bagamoyo hadi katikati ya Jiji.
Kwa Mawasiliano zaidi wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 0800110064 (Bila malipo) au 0735 202 121 (WhatsApp Tu)
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano