TAARIFA KWA UMMA - KUKOSEKANA KWA HUDUMA YA MAJI KWA WAKAZI WANAOHUDUMIWA NA TENKI LA CHANGANYIKENI
TAARIFA KWA UMMA
KUKOSEKANA KWA HUDUMA YA MAJI KWA WAKAZI WANAOHUDUMIWA NA TENKI LA CHANGANYIKENI
23/09/2024
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inapenda kuwataarifu Wananchi na Wakazi wa wateja wanaopata huduma kupitia tenki la Maji Changanyikeni kuwa, kutakuwa na ukosefu wa huduma ya maji kwa muda wa saa 10, siku ya Jumatatu, 23/09/2024 kuanzia saa 7 Mchana hadi 5 Usiku.
Sababu: Kuruhusu matengenezo katika kituo cha kusukuma maji cha Changanyikeni
Maeneo yatakayoathirika ni:
Mtipesa, West River, Down Hill, Camp Verde, Barabara ya Shule, Lastanza, Hekima, Precious, Camp Stone, Goba Hill, Sunset Close, Kachembele, Kantina, Shama, Magufuli, Mji Mpya Barrier na Ng’ambo ya Mto
Wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 0800110064 (Bure) au 0735202121 (WhatsApp tu)
Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano