TAARIFA KWA UMMA - KUKOSEKANA KWA HUDUMA YA MAJI KWA WANANCHI WA MLANDIZI HADI KISARAWE
TAARIFA KWA UMMA
KUKOSEKANA KWA HUDUMA YA MAJI KWA WANANCHI WA MLANDIZI HADI KISARAWE
28.09.2024
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inawatangazia Wateja na Wananchi wanaohudumiwa na mtambo wa kuzalisha maji Ruvu Juu kuwa, kutakuwa na ukosefu wa huduma ya maji kwa wastani wa saa 7 siku ya Jumamosi Septemba 28, 2024 kuanzia Saa 5 Asubuhi hadi Saa 12 Jioni.
Sababu: Kupisha Matengenezo kinga katika kituo cha kupooza umeme Mlandizi kazi inayofanywa na Shirika la Umeme Nchini (TANESCO)
Maeneo yatakayoathirika ni;
Ruvu darajani, Ruvu JKT, Mlandizi, Mbwawa, Visiga, Mile 35, Misugusugu, Kongowe, Soga, Miembe saba, Kwa Mfipa, Mwendapole, Tanita, Kwa Mathias, Kwa Mbonde, Pichandege, Lulanzi, Kibaha, Kiluvya, Kibamba, Mbezi, Magari Saba, Mbezi inn, Mbezi, Kimara,Tabata, Kinyerezi, Kisukuru, Msigani, Maramba mawili, Tabata, Kimara B, Kimara Korogwe, Bucha, Baruti,Ubungo, Kisarawe, Ukonga, Pugu, Uwanja wa ndege, Majumba sita , Kiwalani na Gongo la Mboto na Kisarawe
Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 0800110064 (bure) au 0735 202 121(WhatsApp tu)
Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano