TAARIFA KWA UMMA - KUPUNGUA KWA UZALISHAJI MAJI KATIKA MTAMBO WA RUVU JUU
TAARIFA KWA UMMA
KUPUNGUA KWA UZALISHAJI MAJI KATIKA MTAMBO WA RUVU JUU
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inawataarifu Wananchi na Wateja wanaohudumiwa na mtambo wa kuzalisha Maji Ruvu Juu uliopo Wilaya ya Kibaha kuwa, kumekuwa na upungufu wa huduma kutokana na matengenezo yanayoendelea katika miundombinu ya uzalishaji Maji katika Mtambo.
Kufuatia upungufu wa uzalishaji, maeneo yafuatayo yanapata Maji kwa msukumo mdogo:
Chalinze Mboga, Ruvu Darajani, Ruvu JKT, Vigwaza, Mlandizi, Mbwawa,Visiga, Maili 35, Misugusugu, Kongowe, Soga, Miembe Saba, Kwa Mfipa, Mwendapole, Tanita, Kwa Mathias, Kwa Mbonde, Picha ya Ndege, Lulanzi, Kibaha, Kiluvya, Kibamba, Mbezi, Magari Saba, Mbezi Inn, Mbezi, Kimara, Tabata, Segerea, Kinyerezi, Kisukuru, Bonyokwa, Msigani, Maramba Mawili, Kimara B, Kimara Korogwe, Bucha, Baruti, Ubungo, Magomeni, Ukonga, Uwanja wa Ndege, Kiwalani, Vingunguti, Gongo la Mboto, Pugu na Kisarawe
Tunaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza.
Wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 0800110064 (bure) au 0735 202121 (WhatsApp Tu)
Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano