Wizara ya Maji

Dar es Salaam Water Supply And Sanitation Authority (DAWASA)

TIRA Logo
TAARIFA KWA UMMA - KUPUNGUA KWA UZALISHAJI MAJI MTAMBO WA RUVU JUU
20 Feb, 2025 Pakua

TAARIFA KWA UMMA

KUPUNGUA KWA UZALISHAJI MAJI MTAMBO WA RUVU JUU
 
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inawataarifu na Wananchi na Wateja wanaohudumiwa na mtambo wa kuzalisha Maji Ruvu Juu uliopo Wilaya ya Kibaha kuwa, kutakuwa na upungufu wa  huduma ya maji kwa muda wa Saa 24.

Muda: Februari 19,2025 kuanzia Saa 4 usiku hadi Februari 20, 2025.

Sababu: Kuruhusu matengenezo ya dharura katika mabomba makubwa ya usambazaji ya ukubwa wa inch 24 na 30 katika eneo la Visiga Madafu. 

Upungufu huu wa uzalishaji Maji utapelekea maeneo yafuatayo kupata Maji kwa msukumo mdogo:
 
Chalinze Mboga, Ruvu Darajani, Ruvu JKT, Vigwaza, Mlandizi, Mbwawa,Visiga, Maili 35, Misugusugu, Kongowe, Soga, Miembe Saba, Kwa Mfipa, Mwendapole, Tanita, Kwa Mathias, Kwa Mbonde, Picha ya Ndege, Lulanzi, Kibaha, Kiluvya, Kibamba, Mbezi, Magari Saba, Mbezi Inn, Mbezi, Kimara,Tabata, Segere, Kinyerezi, Kisukuru, Bonyokwa, Msigani, Maramba Mawili, Kimara B, Kimara Korogwe, Bucha, Baruti, Ubungo, Magomeni, Ukonga, Uwanja wa Ndege, Kiwalani, Vingunguti, Gongo la Mboto, Pugu na Kisarawe

Tunaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza.

Wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 0800110064 (bure) au  0735 202-121 (WhatsApp Tu)

Imetolewa na 
Kitengo cha  Mawasiliano