TAARIFA KWA UMMA - MATENGENEZO KINGA KATIKA MTAMBO WA MAJI RUVU CHINI
TAARIFA KWA UMMA
MATENGENEZO KINGA KATIKA MTAMBO WA MAJI RUVU CHINI
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inakusudia kufanya matengenezo kinga katika Mtambo wa Maji Ruvu Chini kwa lengo la kuimarisha huduma kipindi cha Mvua yatakayopelekea upungufu wa huduma ya maji kwa Saa 12 kwa Siku ya Alhamisi Machi 13, 2025.
Muda: Kuanzia Saa 12:00 Asubuhi hadi Saa 12:00 Jioni
Maeneo yatakayoathirika ni;
Bagamoyo, Mapinga, Mabwepande, Bunju, Tegeta, Kunduchi, Mbweni, Boko, Salasala, Goba, Mivumoni, Madale, Kawe, Lugalo, Makongo, Chuo Kikuu UDSM, Mwenge, Chuo Kikuu Ardhi, Kijitonyama, Mikocheni, Msasani, Oysterbay, Masaki, Mwananyamala, Kinondoni, Magomeni, Kigogo, Chang'ombe, Keko, Kurasini, Kigamboni, Airport, Kiwalani, Buguruni, Vingunguti, Ilala hadi Katikati ya Jiji.
Tunaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza.
Wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 0800110064 (Bure) au 0735 202 121 (WhatsApp Tu)
Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano