TAARIFA KWA UMMA - MATENGENEZO YA DHARULA YATAKAYOATHIRI UPATIKANAJI HUDUMA YA MAJI
TAARIFA KWA UMMA
MATENGENEZO YA DHARULA YATAKAYOATHIRI UPATIKANAJI HUDUMA YA MAJI
25.9.2026
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inawatangazia Wateja na Wananchi wa maeneo ya Tabata, Kinyerezi na Ukonga wanaohudumiwa kupitia Tenki la kuhifadhi maji Bangulo, kuwa kutakuwa na ukosefu wa huduma ya Maji kwa Saa 10.
Muda: Ijumaa Septemba 25, 2026 kuanzia Saa 4:00 Asubuhi hadi Saa 1:00 Usiku.
Sababu: Matengenezo ya bomba kubwa la inchi 16 linalohudumia Wananchi kutoka kwenye tenki.
Maeneo yatakayoathirika;
Mongo la ndege, Ulongoni A na B, Kinyerezi, Tabata Segerea, Pondi, Mbuyuni, NSSF, Banana, Stakishari, Gongolamboto, Mazizini, Ukonga, Markaz, Mikongeni, Kibirico, Kipunguni na Kitunda.
Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza
Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 181 (bila malipo) au 0735 202 121 (WhatsApp tu)
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano
