TAARIFA KWA UMMA - MSAMAHA WA FAINI YA KUREJESHEWA HUDUMA YA MAJI (RECONNECTION FEE)
TAARIFA KWA UMMA
MSAMAHA WA FAINI YA KUREJESHEWA HUDUMA YA MAJI (RECONNECTION FEE)
9.10.2026
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inawatangazia wateja wake katika Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani waliositishiwa huduma za maji kutokana na madeni, kuwa katika maadhimisho ya mwezi huu wa Huduma kwa mteja, Mamlaka imetoa msamaha maalum kwa mteja kurejeshewa huduma bila ya kulipa faini ya kurejeshewa huduma (reconnection fee) mara baada ya kulipa deni la bili yake ya maji.
Muda: Ofa itaanza Oktoba 10 hadi 31 Oktoba, 2026.
Wanufaika: wateja ambao wana madeni ya huduma za Maji ndani ya eneo la kihuduma la DAWASA
Usikose ofa hii, lipa deni lako la maji sasa na urejeshewe huduma bila ya kulipa faini.
Endelea kuwasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 181 (bila malipo) na 0735 202 121 (WhatsApp Tu)
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano
