TAARIFA KWA UMMA - MUENDELEZO WA DAWASA MTAA KWA MTAA SASA NI WILAYA YA KINONDONI
TAARIFA MUHIMU
MUENDELEZO WA DAWASA MTAA KWA MTAA SASA NI WILAYA YA KINONDONI
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) inawataarifu Wananchi kuwa awamu ya pili zoezi la DAWASA Mtaa kwa Mtaa inaanza Septemba 19 hadi 21,2024 katika Wilaya ya Kinondoni katika Kata za Wazo na Goba.
Kupitia zoezi hili litahusisha uwepo wa Dawati la huduma kwa mteja katika eneo la Mivumoni katika Tank la Maji Wazo mkabala na Viva supermarket.
DAWASA inawaalika Wananchi wa mitaa ifuatayo:
Madale, Mivumoni, Nakasangwe, Kisanga, Kilimahewa, Lalacha, Modemba, Uwanja wa Nike, Kwa bedui, Makirikiri, Kazi moto, Transforma, Sandawe, Nuru njema, Kaza roho, Uzunguni na Tegeta A .
Wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 0800110064 (bure) na 0735 202 121 WhatsApp tu.
Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano