TAARIFA KWA UMMA - UKOSEFU WA HUDUMA YA MAJI KWA WAKAZI WA UNGINDONI HADI MAWENI - KIGAMBONI
TAARIFA KWA UMMA
UKOSEFU WA HUDUMA YA MAJI KWA WAKAZI WA UNGINDONI HADI MAWENI - KIGAMBONI
21.4.2025
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inawatangazia Wateja na Wananchi wa maeneo ya Ungindoni hadi Maweni wilaya ya Kigamboni kuwa, kutakuwa na ukosefu wa huduma ya Majisafi kwa saa 24 siku ya Jumatatu April 21, 2025 kuanzia Saa 12 asubuhi hadi siku ya Jumanne April 22, 2025 Saa 12 asubuhi.
Sababu: Kuruhusu matengenezo bomba kuu la usambazaji maji lenye ukubwa wa inchi "16" eneo la Ungindoni Kata ya Mjimwema.
Maeneo yatakayoathirika ni;
Uvumba,Kiziza,Ungindoni,Kifurukwe,Mjimwema, na Maweni.
Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 0800110064 (bure) au 0738 096 083 DAWASA Kigamboni.
Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano