TAARIFA KWA UMMA - ZOEZI LA USOMAJI MITA ZA MAJI DAR ES SALAAM NA PWANI
TAARIFA KWA UMMA
ZOEZI LA USOMAJI MITA ZA MAJI DAR ES SALAAM NA PWANI
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inawaatarifu Wateja na Wananchi katika Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, kuwa zoezi la usomaji mita za maji linaanza Oktoba 7 hadi 11, 2026.
Baada ya zoezi la usomaji mita kukamilika, Mteja atapokea ujumbe wa kuhakiki usomaji wa mita yake kabla ya bili kutumwa.
Mambo muhimu ya kuzingatia;
1. Fungua geti au hakikisha mita inafikika kwa urahisi ikiwa ipo ndani ya uzio.
2. Ondoa vizuizi vinavyoweza kuficha au kuathiri usomaji wa mita.
3. Toa ushirikiano wa msomaji mita ili taarifa za matumizi ya maji zichukuliwe kwa usahihi.
4. Hakiki ujumbe mfupi wa simu (SMS) unaotumwa kuthibitisha usahihi wa taarifa za matumizi kabla ya bili kutumwa.
Kwa msaada zaidi wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 181 (Bure) au 0735 202 121 (WhatsApp tu)
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano
