TAARIFA KWA UMMA - ZOEZI LA USOMAJI MITA ZA MAJI KUANZA MACHI 10 - 15, 2025
10 Mar, 2025
Pakua
TAARIFA KWA UMMA
ZOEZI LA USOMAJI MITA ZA MAJI KUANZA MACHI 10 - 15, 2025
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inawataarifu Wateja na Wananchi katika Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, kuwa zoezi la usomaji wa mita za maji linaanza Machi 10 hadi 15, 2025.
Baada ya zoezi la usomaji mita kukamilika, Mteja atapokea ujumbe wa kuhakiki usomaji wa mita yake kabla ya bili kutumwa.
Kwa taarifa zaidi wasiliana nasi kituo cha huduma kwa wateja 0800110064 (Bure) na 0735-202121 (WhatsApp tu)
Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano