Wizara ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)

TIRA Logo
TAARIFA KWA WAKAZI WA MBEZI, LUGURUNI NA KWEMBE
30 Sep, 2026 Pakua

TAARIFA KWA WAKAZI WA MBEZI, LUGURUNI NA KWEMBE

KUKOSEKANA KWA HUDUMA YA MAJI KWA SAA 9

30.9.2026

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inawatangazia Wananchi wa Maeneo ya Mbezi, Luguruni na Kwembe wanaohudumiwa kupitia vituo vya kusukuma maji Mbezi Inn, Kisarawe na Bangulo kuwa kutakuwa na ukosefu wa huduma ya Maji kwa saa 9.

Muda: Oktoba 1, 2026 kuanzia saa 3:00 Asubuhi hadi saa 12:00 Jioni

Sababu: Kuruhusu Matengenezo kinga yanayofanywa na Shirika la Umeme Nchini.

Maeneo yatakayoathirika ni;

Mbezi Inn, Luguruni, Magari Saba, St. Joseph, Mbokomu, Kwa Yusuph, Kwa Mkurugenzi, Luguruni, Ofisi za DAWASA, Kwa Mkwele, Kwembe Kijijini, Tawalani, Ndombele, Amani street, Mchikichini, John Dee.

Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

Kwa taarifa zaidi wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 181 (bila malipo) au 0735 202 121 (WhatsApp tu)

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano