TAARIFA KWA WAKAZI WA MLANDIZI HADI KISARAWE - KUPUNGUA KWA UZALISHAJI MTAMBO WA RUVU JUU
TAARIFA KWA WAKAZI WA MLANDIZI HADI KISARAWE
KUPUNGUA KWA UZALISHAJI MTAMBO WA RUVU JUU
23.10.2026
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inawatangazia wateja na wananchi wanaohudumiwa na mtambo wa kuzalisha maji Ruvu Juu uliopo Mlandizi Mkoani Pwani kuwa, kumetokea itilafu ya Pampu hali itakayopelekea upungufu wa huduma ya maji kwa baadhi ya maenei yanayohudumiwa na Mtambo huo.
Hali hii itapelekea upatikanaji wa maji chini ya kiwango na hafifu kwa Wakazi wanaotegemea Mtambo wa Ruvu Juu
Muda: Saa 3 asubuhi hadi saa 3 usiku
Maeneo yatakayoathirika;
Ruvu Darajani, Ruvu JKT, Vigwaza, Mlandizi, Mbwawa, Soga, Mwendapole, Tanita, Kwa Mathias, Picha ya ndege, Kibaha, Kiluvya, Kibamba, Malamba mawili, Mbezi, Kimara, Tabata, Segerea, Kinyerezi, Kisukuru, Bonyokwa, Ukonga, Uwanja wa ndege, Kiwalani, Vingunguti, Gongolamboto, Pugu na Kisarawe.
Tunaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza
Kwa maelezo tupigie; Kituo cha huduma kwa wateja 181 (Bila Malipo na 0735 202 121 (WhatsApp tu)
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano
