Wizara ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)

TIRA Logo
TAARIFA KWA WAKAZI WA TEGETA, GOBA NA MSUMI - MATENGENEZO YA DHARURA YATAKAYOATHIRI UPATIKANAJI HUDUMA YA MAJI
27 Sep, 2026 Pakua

TAARIFA KWA WAKAZI WA TEGETA, GOBA NA MSUMI

MATENGENEZO YA DHARURA YATAKAYOATHIRI UPATIKANAJI HUDUMA YA MAJI

27.9.2026

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inawatangazia Wateja na Wananchi wa maeneo ya Tegeta, Goba na Msumi kuwa kutakuwa na ukosefu wa huduma ya Maji kwa Saa 10.

Muda: Jumapili Septemba 27, 2026 kuanzia saa 6:00 Mchana hadi saa 3:00 Usiku.

Sababu: Matengenezo ya bomba la inchi 8 kwenye air valve katika maeneo ya Lugalo.

Maeneo yatakayoathirika ni;

Tegeta A, Goba, Matosa, Uzaramoni, Contena, Msumi, King'ongo, Mbilinyi, Tangi bovu, IPTL, Mama Mfinanga, Kwa Mpemba, Kawe, Seduta, Mbezi Beach A, Mbezi Beach, Kilonga Wima, Madini na Kunduchi.

Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 181 (bila malipo) au 0735 202 121 (WhatsApp tu)

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano