Wizara ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)

TIRA Logo
TAARIFA KWA WAKAZI WA TEMEKE NA MBAGALA - MABORESHO YA MIUNDOMBINU YA UMEME YATAKAYOATHIRI UPATIKANAJI WA MAJI WILAYA YA TEMEKE
25 Jun, 2026 Pakua

22.06.2026

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inawatangazia Wananchi na wakazi wanaohudumiwa na mtambo wa uzalishaji maji Mtoni kuwa kutakuwa na ukosefu wa huduma ya maji kwa muda wa saa 7 kwa siku ya Jumatatu 21/06/2026 kuanzia saa 6:00 Mchana hadi saa 1:00Jioni

Sababu: Kuruhusu matengenezo katika miundombinu ya Umeme yanayofanywa na Shirika la Umeme Nchini.
 
Maeneo yatakayoathirika ni;

 TEMEKE: katika maeneo ya Kinesi, Vianiza, Kimicho, Mtoni Mtongani, Mtoni Aziz Ally, Mtoni Kichangani, Tandika Azimio Kusini, Azimio Kaskazini, Kijichi, Mbagala Sabasaba, Mwinyimaki, Maputo, Bibidua, Msomeni, Mtoni Unguja, Dawasa Kota, Dawasa Sokoine, Transfoma la Sokoine, Tandika Sokoni, Tandika Plaza, San Diego,  Akiba Bank, Mapipa,  Mbagala Makuka, Mbagala Bughudadi,  Mbagala Mwisho, Zakiem, Mbagala Kibonde Maji, na Mbagala rangi tatu.

Tunaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza.

Wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 181 (bure) au 0735 202-121(WhatsApp tu)

Imetolewa na 
Kitengo cha Mawasiliano