TAARIFA KWA WAKAZI WA WAZO HADI MADALE - MATENGENEZO KINGA YATAKAYOATHIRI UPATIKANAJI HUDUMA YA MAJI
TAARIFA KWA WAKAZI WA WAZO HADI MADALE
MATENGENEZO KINGA YATAKAYOATHIRI UPATIKANAJI HUDUMA YA MAJI
19.10.2026
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inawatangazia Wateja na Wananchi wa maeneo Wazo hadi Madale wanaohudumiwa na kituo cha kusukuma maji Wazo kuwa kutakua na ukosefu wa huduma ya Maji kwa saa 8.
Sababu: Kuruhusu matengenezo kinga katika Miundombinu ya mfumo wa umeme yatakayoathiri uendeshaji katika kituo cha kusukuma maji Wazo.
Muda: Jumanne, Oktoba 20, 2026 kuanzia saa 3:00 Asubuhi hadi saa 11:00 Jioni.
Maeneo yatakayoathirika;
Wazo Mkanada, Kwa Makamba, Wazo Mashamba ya Jeshi, Wazo Bwawani, Wazo Kizunga, Umoja Road, Wazo Kontena, Mivumoni, Nyakasangwe, Kinondo East, Wazo Engineering, AKG Glitters, Mika Meat, Felix Mlaki (Saria hall and hotel), Mshale Tanzania, Tegeta A pamoja na Wazo Booster 1&2
Tunaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza
Kwa maelezo tupigie; Kituo cha huduma kwa wateja 181 (Bila Malipo) na 0735 202 121 (WhatsApp tu)
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano
