TAARIFA YA DHARURA - UKOSEFU WA HUDUMA YA MAJI KWA WAKAZI WA KIMARA HADI MBEZI
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inawatangazia wateja na Wananchi wa maeneo ya Kimara suka, Kwa msuguri, Kimara temboni, Kimara B, Kibanda cha Mkaa na Mbezi kuwa kutakuwa na ukosefu wa huduma ya maji kwa saa 24 kuanzia tarehe 10.5.2024 hadi Tarehe 11.5.2024.
Sababu: Kuruhusu matengenezo kwenye bomba kubwa la usambazaji maji la inchi 24 eneo la Kimara Suka
Wataalamu wa DAWASA wanaendelea na matengenezo na jitihada za haraka kurejesha huduma ya maji kwa wakazi walioathirika na hitilafu hii.
Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja
0800110064 (Bure)
0735 451865 (DAWASA Ubungo)
0735 202121 ( Whatsapp tu)
Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano