TAARIFA YA UTEKELEZAJI MRADI WA MAJI MSUMI
TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MRADI WA MAJI MSUMI
Mradi wa Maji Msumi kwa Kutumia Tanki la Tegeta A katika Mtaa wa Msumi - Kata ya Mbezi. Gharama ya mradi ni TZS 1,823,941,267.27 pamoja na VAT. Mradi huu unatekelezwa na fedha kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mradi huu ni sehemu ya jitihada za Serikali kuhakikisha upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa wakazi wa Wilaya ya Temeke unakuwa wa uhakika kwa nyakati zote. Mradi huu ulianza tarehe 17/04/2025 na unatarajia kukamilika tarehe 30 Septemba 2026. Mradi huu unagusa kigezo cha 5.0 kipengele 5.4 kinachoeleza jinsi Halmashauri inavyoshikiana na Mamlaka za Maji na Wananchi kuboresha huduma ya maji na upanuaji wa huduma za maji kwa wananchi.
KAZI ZILIZOTEKELEZWA
1. Kazi zilizotekelezwa ni ulazaji wa bomba za usambazaji maji zenye kipenye cha inchi 1.5 hadi 8, Ujenzi wa Sump, Pump house, ujenzi wa Mnara (Kioski), Ufungaji umeme, Transformer na Pampu.
2. Kazi ya Ulazaji bomba za usambazaji maji za Mradi imefanywa na vibarua, kazi ya Ufungaji umeme, Transformer na Pampu imefanywa na Mzabuni Rosel International Limited, kazi ya Ujenzi wa Pump house, ujenzi wa Mnara (Kioski) na Vizimba.
MANUFAA YA MRADI
Mradi huu una manufaa kwa wananchi kama ifuatavyo: -
1. Mradi unaenda kuongeza upatikanaji wa maji safi na salama kiasi cha lita 2,160,000 za maji kwa siku, hivyo kupunguza adha ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa wakazi wa Mtaa wa Msumi.
2. Mradi utanufaisha jumla ya watu 18,000 kutoka katika Mtaa wa Msumi, Kata ya Mbezi, Wilaya ya Ubungo.
